SEHEMU YA A.
MATUMIZI YA LUGHA(Alama 40)
a. Andika sifa mbili mbili za sauti zifuatazo. (alama 2)
(i). /e/
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
(ii). /ch/
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
b). Unda maneno yenye muundo ufuatao wa sauti. (Alama 2)
KIKIKI………………………………………………………………………………………..
IKKI……………………………………………………………………………………………
c). Onyesha miundo miwili ya nomino katika ngeli ya U-ZI (alama 2)
…………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..
d). Tunga sentensi moja moja kuonyesha matumizi ya viakifishi vifuatavyo. (alama.2)
i). Vifungo …………………………………………………………………………………
ii). Kibainishi ……………………………………………………………………………..
e). Bainisha aina za virai vilivyopigiwa mstari (alama 2)
Mhadhara huo tata ulitolewa jana jioni.
…………………………………………………………………………………………………
f). Andika sentensi ifuatayo katika ukubwa. (Alama 2)
Ndege hao wana manyoya mengi
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
g). Andika visawe vya maneno yafuatayo. (Alama 2)
i). Doa
…………………………………………………………………………………………………
ii). Omba
…………………………………………………………………………………………………
(h) Tunga sentensi moja kutofautisha maana ya riti na ridhi (Alama 2)
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
i). Bainisha silabi katika neno (Alama 1)
Wanyweshavyo
…………………………………………………………………………………………………
j). Bainisha kiima na chagizo katika sentensi ifuatayo (alama.2)
Mwenyewe alikipenda kwa dhati
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
k). Tumia kielezi cha kiasi badala ya kile kilichopigiwa mstari. (alama.2)
Msichana yule alizungumza kitausi.
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
l). Geuza sentensi ifuatayo katika usemi halisi (alama.2)
safina alimwambia Asha kuwa angetembelea wazazi wao siku hiyo jioni.
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
m). Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha matawi (Alama 3)
Mvua kubwa inayonyesha itasababisha mafuriko.
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
n). Kanusha sentensi ifuatayo kwa wakati ujao hali ya kuendelea (Alama 2)
Walimu wanafunza
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
o). Andika upya setensi ifuatayo wa kuzingatia kauli iliyowekwa katika mabano (Alama 2)
yeye ni bahili itakuwa vigumu kumkopesha pesa. (kutendesheka)
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
(p) Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi mawili tofauti ya ‘na’ (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
q). Andika sentensi ifuatayo upya ukianzia yambwa tendewa (alama.2)
kirwa alimjengea mama huyo nyumba kwa mawe
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
r). Ainisha vishazi katika sentesi ifuatayo. (alama 2)
ingawa alitia bidi masomoni,alifeli mtihani.
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
s). Andika sentensi upya ukitumia vinyume vya maneno yaliyopigiwa mstari. (Alama 2)
Mama alijitwika kikapu mgongoni baada ya kuinjika chungu mekoni.
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
t). Andika sentensi zifuatazo upya kwa kufuata maagizo uliyopewa.
i). umekuja (alama 2)
ii) Tumefurahi sana (unganisha sentensi hizi kwa kuanza na kuja…….)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
SEHEMU YA B: USHAIRI- (Alama 20)
Niokoa muokozi, uniondolee mashaka
Kuyatukua siwezi, mjayo nimedhikika
Nimekitiri simanzi,ni katika kuudhika
Mja wako nasumbuka,nipate niyatakayo
Mja wako nasumbuka,nataka kwao afua
Nirehemu kwa haraka,nami nipate pumua
Naomba hisikitika,na mikono hiinua
Mtenda ndiwe moliwa,nipate niyatakayo
Mtenda ndiwe moliwa,we ndiwe mola wa anga
Mazito kuyaondoa,pamoja na kuyatenga
Ukauepusha ukiwa,ya pingu zilonifunya
Nikundulia muwanga,nipate niyatakayo
Nikundulia muwanga,nipate toka kizani
Na huzuni n’ondolea,itoke kwangu moyoni
Mambo mema niegheshea,maovu nisitamani
Nitendea wa manani,nipate niyatakayo
Igeuze yangunia,dhaifu unipe mema
Nili katika dunia,kwa afia na uzima
Moliwa nitimizia,yatimize yawe mema
Nifurahike mtima,nipate niyatakayo.
Maswali
(a). Eleza bahari zozote mbili za shairi hili (alama 4)
(b). Eleza muundo wa shairi hili (Alama 4)
(c). Mshairi ametumia uhuru wake wa utunzi. Eleza mifano minne huku ukitoa mifano (alama 4)
(d). Andika ubeti wa pili katika lugha tutumbi (alama 4)
(e). Fafanua dhamira ya mtunzi wa shairi hili
(alama.2)
(f). Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumika katika shairi (alama 2)
(i). Nimedhihika
(ii). Nifurahike mtima
SEHEMU YA C: RIWAYA – ASSUMPTAMATEI - CHOZI LA HERI
Jibu swali la 2 au 3:
2. Haki za watoto hazitiliwi maanane katika jamii nyingi za kiafrika. Eleza ukweli wa kauli hii
kwa kurejelea Riwaya ya chozi la heri (Alama 20)
au
3. “Kuukata mkono niliostahili kuubusu yalinifika ya kunifika”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili (Alama 4)
b. Eleza namna msemaji alivyoukata mkono aliostahili kuuibusu. (alama 6)
c. Eleza tamathali ya usemi unaojitokeza katika dondoo hili. (alama.2)
d. Fafanua sifa nne za msemaji wa kauli hii (alama 8)
SEHEMU YA D : FASIHI SIMULIZI
Jibu swali la 4 au 5
4. (a) Miviga ni nini? (Alama 2)
(b) Fafanua sifa sita za miviga (Alama 6)
(c) Kwa nini jamii huthamini miviga (Alama 8)
(d). Onyesha udhaifu unaohusishwa na miviga (Alama 4)
Au
5. i. Fafanua sifa tano za hekaya. (Alama 5)
ii. Eleza maana ya; (alama 5)
a. Vitanza ndimi.
b. Tahalili
c. Vivugo
d. Matambiko
e. Maapizo
iii. Jadili mifano mitano ya ngomezi za kisasa. (al 5)
iv. Eleza kwa hoja tano udhaifu wa hojaji kama njia ya kukusanya Fasihi Simulizi. (al 5)